Categories
Gospel Social, economic & Political insights.

Maisha Ni Rahisi

Tuna uwezo wa kusababisha maisha mema.

https://anchor.fm/jessecameathi.com/episodes/Maisha-Ni-Rahisi-eu9ghp

Si wazo njema kufanya maisha kuwa magumu zaidi ya vile yalivyo. Ni bora kufahamu kwamba una uwezo wa kuzuia mabaya kukufanyikia kwa kujizuia kutenda matendo ambayo yangesababisha kilio kwako. Jua kwamba yote unayoyapitia, kwa njia moja ama nyingine umechangia pakubwa kuyasababisha bila ya kujua. Una uwezo wa kufanya maisha yawe jinsi unavyotaka kwa kuwa na mtazamo mwema wa maisha. Cha msingi ni kuhakikisha kwamba dhana yako si potovu na kujizuia kuwaza mawazo ambayo yanaweza kukuelekeza kutenda mambo yaletayo maafa. Maisha Ni Rahisi, tusiyafanye yawe magumu. Tusipotii tutapitia magumu kwa sababu anayetuambia tutii anataka tuwe na wakati mwema na anajua tusipotii tutapitia wakati mgumu sababu mambo hayataingiana inavyofaa. Kupinga ukweli Ni kama kupiga ngumi ukuta sababu hakuna siku utaweza kuhalalisha uongo. Hakuna siku maji yataitwa mawe na hakuna siku mawe yataitwa maji. Hakuna siku shetani atakuwa Mungu na Mungu hawezi kuwa shetani. Hakuna siku giza litawiana na mwangaza. Maisha ni rahisi, wacheni kuyafanya magumu mkikataana na ukweli ambao unaonekana wazi kabisa. Wacheni kutafuta njia mbadala wakati njia sahihi Haina kasoro na haijafeli wenye haki. Usipotii , maisha Ni magumu. Ukitii, Maisha ni rahisi. Mimi Jesse Kimathi naona afadhali kutii badala ya kupiga ngumi ukuta na kuumiza mkono wangu. Unaposkiza hili shairi natarajia mtazamo wako kuhusu maisha ni wa ukweli.

https://anchor.fm/jessecameathi.com/episodes/Maisha-Ni-Rahisi-eu9ghp

By jessecameathi

Writer and artist from East Africa.

2 replies on “Maisha Ni Rahisi”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s