Ironically wenye wanasema hawapangwingi ndio maisha imewapanga kwelikweli

Mnajua the kind of guys wenye wanapanganga watu wa sipangwingwi. Niko na kabeshte flani kanashindanga kakisema hakapangwingi kama ngui lakini kajamaa kanapangangwa kila siku. Kwanza kanaendanga kibarua ya kutrim maua kwa fence za wadosi huko Karen. Kakiitisha mshahara kanapangwa wiki mzima kakiambiwa kangoje.

Kanatumanga fare kwa kidem flani kinakapanga kikikaambia kinakuja kinakuja hadi siku inaisha. Kajamaa bado ni kamsanii kanambiangwa kuja show hapa club Rising kanaenda kanabamba watu mpaka che halafu kanaambiwa eti kamelipwa na exposure. Kamorio kalivutia bangi chuom flani kanairo kakashikwa kakapelekwa Central kakaa cell wiki mzima na juu hakananga simu kalinimanage kuomba karao simu nikamtumia ruabe akakaachilia.

Kajamaa kanakuliwangwa na njaa kakiskia vinanda za harusi zikilia kanakimbia uko kakijua wazi Kuna free food kakifika uko kanapangwa kwa line refu ndio kakule halafu baadae kanaambiwa kasaidie kupeleka viti kwa kanisa na kuweka vyombo zilizotumiwa mahali moja. Kaman Kako na roommate mngori anakapiganga exile kila wikendi halafu tym amepeka ugali nyama anakapeanga githeri chemsha akikaambia ili siku katachanga pesa ya nyama na unga ndio kanaweza complain.

MCA flani alikatumia kusambaza poster zake za campaign four years ago na kitu akikapea ni mzinga ya konyagi. Kamorio kanasema hakawezi ajiriwa eti hakapangwingi saizo hata biashara hakana ni handouts kanapatiwa na wenye wameajiriwa na kabla wakapatie lazima kachimbe shimo kama tatu hivi kawapandie migomba ya mandizi waje wavune na wajivunie huku kakisema hakapangwingi. 

Leave a Reply