Kama hujajipanga kubali upangwe

Usiwe mtu ambaye hawezi kusaidika. Usiwe mwanadamu anayetaabika bila ya kuomba msaada sababu ya kuhofia kuaibika.

Kama mambo yameharibika na kwenda segemnege usikae ukisubiri muujiza utendeke kwa sababu yatazidi kwenda mrama. Lolote utakalo kufanikisha maishani lina gharama.

Saa zingine gharama hiyo ni kunyenyekea, kukubali umeshindwa na kuitisha msaada. Kwa sababu ada ya mja hunena muungwana ni kitendo utawajua wale ambao utakimbilia kuomba msaada kwa matendo yao.

Usiendelee kupiga ngumi ukuta na kuharibu mkono wako ilhali we ni mshindani unapokubali kushindwa. Kuwa mtu ambaye anaweza chukuana na shepu yeyote kama maji kwa kukubali kupindwa ndio uweze kuingiana na hali ambayo itakunufai na inufai jamii kwa jumla.

Maisha ni mabadiliko ndio maana yabidi ubadilike jinsi nyakati zinavyobadilika ndio usikwamwe katika matukio ya zamani.

Saa zingine si vibaya kupangwa. Kama huna kazi kubali upewe kazi. Kama umeishiwa na maarifa kubali maarifa yasiyo ya kupotosha. Kama huna gari na Kuna mwenzio yuataka kukubeba bila kuitisha malipo kubali msaada huo. Kama umekosea ukakosolewa kubali kuondoa kasoro. Usiwe mtu wa kujipiga kifua na kusema ‘hupangwingwi’ ilhali maisha yamekupanga unalala njaa, hauna mavazi mazuri na unalewa chakari. Kuwa mtu asiye penda kusifiwa kwamba hana kasoro.

Saa zingine kupangwa na waja si jambo nzuri lakini kila wakati kupangwa na Mungu ni jambo nzuri liletalo furaha na amani moyoni kwa hivyo usijivune kiasi kwamba huwezi kuitisha msaada wa Mungu kwa sababu Mungu ndiye aifanyayo dunia izunguke. Fuata nyayo zake zitakuelekeza kwenye uzima wa milele.

Kuhusiana na hayo nina shairi lifuatalo;