Maisha ni kujifanya, Usipojifanya utafanywa

Maisha ni kujifanya. Usipojifanya utafanywa. Lazima ujifanye uwe namna ambayo inakufaa. Utakuwa kile ambacho utajifanya uwe kwa hivyo usiwajali wale watakaosema unajifanya kwa sababu wameona kuna jambo ambalo umeanza kufanya na kwa kuwa hawataki ufanikiwe kulifanya watasema unajifanya ndio uvunjike moyo kama nia yako ni kuwaridhisha. Lakini kama nia yako si kuwaridhisha, endelea kujifanya mpaka ufanikiwe.